RIWAYA YA MFUNGWA

SEHEMU YA 1
                                                               RIWAYA YA MFUNGWA
                 10/11/2016
               Ni saa kuminambili jioni,ndani ya gereza la segerea jijini dar es salaam,wafungwa wametulia ndani ya vyumba vyao huku kila mmoja akiwaza juu ya maisha yake binafsi.Ukimya uliokuwa umetawala ulifanya sauti ya viatu vikitembea iweze kusikika kwa urahisi kwa wafungwa wale,sauti ile ilizidi kusogeakaribu zaidi na vyumba vile vya wafungwa,wafungwa wote waligeuza vichwa vyao na kutazama mlango wa chuma uliokuwa na matundu ili waweze kumuona yule mtu aliyekuwa akija.Baada ya sekunde kadhaa sura ya kijana mweusi,mwenye kifua kikubwa na mrefu kidogo ilionekana mbele yqa mboni ya macho ya wafungwa wale.Kijana yule alionekana akijaribu kuwahesabu wafungwa wale kwa kutumia kidole chake cha mkono wa kulia,mkono wa kushoto alikuwa na kidaftari kidogo ambacho alioneka akikitumia kuandika kitu fulani na pengine ni idadi ya wafungwa waliokuwa ndani ya chumba kile.Baada ya kumaliza kuandika,alimuita askari mwenzake ambaye alikuja na bunduki aina ya smg,iliyokuwa mgongoni kwake,askari yule wapili alipofika alifungua mlango wa chumba kile na wafungwa wote waliamliwa kutoka nje mara moja.


            Ulikuwa ni muda wa ibada katika gereza la Segerea,wafungwa wa dini ya kiislamu walikwenda mahali pao pa kufanyia sala,na wakristo hivyo hivyo.Ibada zilichukua muda wa takribani nususaa hivi,na ndipo wafungwa walirudishwa ndani ya vyumba vyao ambavyo walivitumia kulala,Joto kali lililosababishwa na madirisha madogo ya chumbakile yalimfanya kila mfungwa avue shati lake na kubaki kifua wazi.Vifua vyao vilionyesha kuwa wamekuwa wakifanya kazi kubwa na nzito kwa kipindi kirefu sana hali iliyopelekea miili yao kukomaa sana.Miongoni mwa wafungwa hao,alikuwemo Kijana mmoja mwenye umri wa takribani miaka 19 mpaka 22 hivi,alionekana kuwa ni mdogo sana kiumbo kulinganisha na wafungwa wengine.Kutokana na umbolake dogo wafungwa wengi walipenda sana kumuonea,kwani walijua fika kuwa asingeweza kuwafanya chochote,kijana huyo aliitwa Michael Mbando,alionekana kuwa mpole sana na hakuna mtu aliyewahi kujua kwamba ni nini kilimfanya kijana yule awekwe gerezani.Sikumoja wakati wa usiku kijana Michael Mbando alianza kukashifiwa na wafungwa wengine huku wakimdhihaki kwa kumuita mtoto wa mama,hali ile ili mtia hasira sana Michael lakini alijaribu kwa hali mali kujizuia hali iliyompelekea kumwaga machozi.
"oyaa acha kulialia kitoto hapa,wengine tumehukumiwa kifungo cha maisha ati sembuse wewe miaka 8 tu"aliongea mbabe mmoja wa gereza lile huku akimshika Michael shavuni,jambo lile lilimuudhi na kumkera sana Michael hali iliyompelekea kupandisha hasira na kuamua kutwanga kofi mfungwa mwenzake aliyekuwa akijaribu kumshika.Ugomvi mkumbwa ulizuka baina ya wafungwa walewalipigana vikali huku asikali aliyekuwa amesimama nje ya chumba kile akijaribu kuwatuliza.


        11/11/2016
          Ndani ya gereza lile kulikuwa na utaratibu uliokuwa umewekwa na wafungwa wale yakuwa kila ifikapo muda wa kulala ni lazima mfungwa mmojawapo awasimulie hadithi yakweli ya maisha yake au pengine ya kutunga.Katika kipindi hicho cha simulizi wafungwa walikuwa wanakuwa watulivu sana,usingesikia kelele wala maongezi yoyote kwakuwa wengi walikuwa wakihuzunika au wakifurahia hadithi kutoka kwa wafungwa wenzao.Siku hiyo ilikuwa ni zamu ya Michael kusimulia hadithi yake,hivyo aliwaomba wafungwa wenzake wamtegee masikio kidogo iliaweze kuendele na simulizi aliyoitunga yeye mwenyewe...
"haya naombeni mnisikilize,leo ninawasimulia hadithi niliyoitunga mimi mwenyewe"alisema Wilson huku akimtizama mfungwa mwenzake aliyekuwa amenyosha mkono huku akionyesha ishara ya kutaka kunena jambo fulani.
"karibu said"alisema Wilson huku akimkaribisha yule kijana aseme alichokuwa anataka kusema.
"Najua kaka wilson unajua sana kutunga hadithi lakini mimi ningeshauri tuwe tunasimuliana hadithi zenye uhalisia kwenye maisha yetu"
"Unamaanisha nini?"waliuliza wafungwa wengine.
"Namaanisha kwamba,sisi sote ni wafungwa na kilamtu amekuja humu kutokana na kosa fulani alilolifanya,na sio hivyo tu kunawengine humu wamesingiziwa na kupewa kesi zisizo zao.Kwahivyo ni bora tusimuliane visa vilivyopelekea sisi kukutana hapa leo"alisema yule kijana huku akiwaangalia wenzake.Wafungwa wote walionekana kulifurahia sana wazo lile,wafungwa wote walibaki wakimuangalia Wilson huku wakisubiria kusikia kisa kilichomfanya atumikie kifungo hicho.Wilson alijiinamia chini kwa sekunde kadhaa kisha akainua shingo yake na kuwatazama wenzake"Kisa changu ni kirefu sana na sidhani kama ninaweza kukisimulia chote siku hii ya leo"alisema Wilson huku akiwatizama wafungwa wenzie.Aliinamisha kichwa chini kwa mara ya pili na kisha kufuta machozi yake kwa kutumia nguo yake iliyokuwa imechakaa sana ,aliwatizama wenzake huku akiwa hajui aanzie wapi kuwasimulia wenzake.

      "Mimi ni Michael ,nimezaliwa katika familia ya wazazi wawili waliokuwa ni walemavu,babayangu alikuwa ni mlemavu wa ngozi na mama yangu alikuwa ni mlemavu wa macho,alikuwa kipofu.Nilianza kuishi maisha mabaya tangu nikiwa tumboni mwa mama yangu,Mama yangu hakuwa na uwezo wa kupata mlo wa kilasiku hata kipindi nilipokuwa tumboni mwake,Ndugu wa wazazi wangu wote walikuwa na uwezo kifedha lakini hawakuwa tayari kuwasaidia kwa chochote kitu.Mama na baba yangu waliishia kulala njaa mara kwa mara ,walimuomba mungu kila kukicha wakimtaka awape maisha mazuri na yenye furaha tele,lakini sala zile zilikuwa zikiwarudia kinyume hali iliyowapelekea kupoteza imani yao katika maombi

Comments