Ni miaka kadhaa imepita tangu sekeseke la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) lianze kushamiri na kushika kasi hapa nchini na baadhi ya nchi jirani pia.Watu hawa maisha yao yamekuwa yako hatarini kwa kipindi kirefu sana hali inayowapelekea wao kuwa na fikra za kujiona kama wako tofauti na watu wengine.
Watu hawa wenye ulemavu wa ngozi wamekuwa wakiishi kwa hofu sana kutokana na ulinzi wao kuonekana kuwa mdogo.Serikali kwa kiasi kikubwa imekuwa ikijitolea kuwalinda kwa kiasi kikubwa japo kuna baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiwauwa watu hawa kwa nadharia kuwa watajipatia utajiri mkubwa kupitia viungo vyao.
Hali hiii iliendelea kushika kasi hapa nchini,serikali na baadhi ya mashirika binafsi yalijaribu kupigana vikali na watu wanaowauwa Albino.Ni dhahiri kwamba asilimia kubwa ya wahusika wa matukio haya wamekuwa hawakamatwi na polisi ni hii ni kutokana na baadhi ya jamii kuwaficha waharifu hawa,hii imekuwa ni tatizo sana.
Waganga wa kienyeji wamesemekana kuwa ndio washinikizaji wakubwa wa mauwaji haya ya kinyama kwakuwa wamekuwa wakiwaaminisha watu wanaweza kupata utajiri kupitia viungo vya albino.
Ni wakati wetu sasa kama jamii kuamuwa kupigana vita dhidi ya imani potofu na za kishirikina kama hizi.Ni ushahuri wangu tu kwa jamii tuweze kushirikiana na vyombo vya usalama katika vita dhidi ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Comments
Post a Comment