WASABABISHAO ONGEZEKO LA WATOTO WA MTAANI NI WAZAZI WENYEWE

          Malezi ya wazazi kwa watoto wao yamekuwa ni changamoto kubwa kwa maisha ya sasa,wazazi wengi wameshindwa kuyatimiza wajibu wao huku sababu kubwa ikiwa ni majukumu ya kikazi lakini pia hata utandawazi.
           Wazazi wengi kutokana na ukuaji wa utandawazi wamejikuta wakijikita sana katika malezi yaliyo jaa utamaduni wa kizungu.Wazazi wengi wameuacha uhusika wao na kujikuta wakiwa watumwa kwa watoto wao.Wamekuwa wakijishusha sana kwa watoto wao,hali inayopelekea watoto hao kuwa katika hali ngumu ya kutokujitambua.
           Wazazi wengi wa sasa wameamua kuzitumia tamaduni za kizungu katika malezi ya watoto wao,mtoto anaomba anunuliwe simu ya bei kubwa na haipiti siku mbili tayari analetewa simu yake.Watoto wengi wa sasa wamekosa uwezo wa kujitambua kutokana na malezi mabaya wanayopata kutoka kwa wazazi wao,mtoto wa kike wa umri kati ya miaka sita kwa sasa anaweza kukuelezea mwanzo mpaka mwisho wa matumizi ya simu.
           Hali hii inapelekea kuongezeka kwa watoto wa mtaani endapo wazazi wa mtoto husika watapatwa na mauti.Pia kuna baadhi ya watoto kutokana na kukosa bahati ya kulelewa katika maadili mema basi anajikuta tayari anajiamini kuwa anajua kila kitu ali inayompelekea hata kujihusisha na maswala ya kimapenzi.Kutokana na hali hii watoto wengi wamekuwa wakizaa katika umri mdogo na kuamua kuwatupa watoto wale ili kuepukana na aibu.

          Hali hii imekuwa chachu kubwa katika ongezeko la watoto wa mitaani hususan katika nchi za afrika hususani Tanzania.Hivyo basi nipende kuwashauri wazazi wawape watoto wao malezi bola na yenye manufaa katika maisha yao.
   by lameck mugisha

Comments