LUCA BERARDI,NI MFANO WA KUIGWA

  Luca Berardi ni miongoni mwa vijana wadogo wenye maumivu makali sana juu ya maovu yatendwayo na wanadamu juu ya wanyama na mazingira yote.Luca Berardi ni raia wa kenya lakini ni chotara kati ya mzungu na muafrika.

   Tangu akiwa mdogo luca alionyesha dalili zote za kuonyesha kupenda sana na kujali mazingira,alipenda sana wanyama na hakufurahishwa na stori zilizokuwa zikiendelea juu ya mauwaji ya tembo na uchomaji wa misitu,

  Hivi tunavyoongea tayari Luca ameanzisha taasisi yake inayojihusisha na maswala ya mazingira,taasisi hiyo imepewa jina la YOUNG ANIMAL RESCUE HEROES(YARH),na inamakazi yake nchini kenya.Taasisi hii inajihusisha na maswala( Recycle)yaani wanachukua taka na kuziweka katika mfumo wa tofauti ambapo zitaweza kutumika tena.Mfano -wanachukua chupa za plastiki zilizotupwa na kuzitumia kutengeneza ndoo za plastiki.


   Pamoja na hayo yote Luca Berardi pia ni msanii wa muziki ,anaimba na kupiga kinanda ,tayari anazo nyimbo kibao ambazo zimemtambulisha vyema ndani na nje ya nchi yake.

           MUNGU IBARIKI AFRIKA,MUNGU MBARIKI LUCA BERARDI.
              By Lameck mugisha.

Comments