SHENZI SANDILE, TAJIRI MWENYE UMRI MDOGO SOUTH AFRIKA.

         Akiwa na umri kumi na minane kijana Shenzi Sandile alikuwa akiendelea kuchukua masomo yake kai ya moja ya vyuo vikuu nchini south afrika. Shenzi alikuwa akiendelea na masomo yake kutokana na shurti la wazazi wake,yeye mwenyewe anasema hakuwahi kupenda kusoma bali aliamini kuwa anauwezo mkubwa wa kubuni biashara itakayomuwezesha kupata pesa.
     
        Baadaa ya miaka kadhaa Shenzi aliamua kuanza biashara akiwa palepale chuoni, aliuza vitu kama keki na vitafunio vingine, biashara hiyo ilionekana kuwa ni ya mafanikio sana kwake hali iliyompelekea kijana Shenzi Sendile kutumia pesa aliyokuwa amepewa kama malipo ya ada na kuifanya kuwa mtaji wake,aliacha shule.

        Baada ya Shenzi Sendile kuamua kuacha shule alijikuta akiingia kwenye mgogoro mkubwa na familia yake, hakuna aliyekuwa upande wake. Shenzi alifanya kazi kwa bidii sana, mtaji wake uliongezeka hali iliyopelekea kufungua biashara ya kuuza nguo, kutokea hapo Shenzi aliendelea kuwa ni kijana mwenye mafanikio sana.

      Akiwa na umri wa Zaidi ya miaka 20 Shenzi aliamua kufungua taasisi inayotoa mafunzo juu ya ujasiriamali kampuni hiyo iliitwa GLOBAL FOREX INSTITUTE ambayo inamakazi yake nchini South Africa, lengo ilikuwa ni kuwahimiza vijana kufanya kazi, kutokukata tamaa na kuwa wabunifu sana. Kijana Shenzi amefanikiwa kuwagusa watu wengi kutokana na hadithi ya maisha yake kwani hivi sasa Shenzi ni miongoni mwa watu matajiri wenye umri mdogo barani Afrika.


 




 by
lameck afrika
C.E.O fikra media group.

Comments