VIJANA WA KITANZANIA WANAOTENGENEZA PESA KUPITIA INTERNET,NA MITANDAO YA KIJAMII.

Mitandao ya kijamii imekuwa miongoni mwa vitu vilivyoleta mabadiliko makubwa katika jamii yetu hususan kwa vijana au watu wa rika dogo. Wapo vijana wengi wa Tanzania au nje ya Tanzania wamenufaika sana kupitia matumizi yao mazuri ya internet au mitandao ya kijamii. Ufafanuzi. Unapozungumzia internet unakuwa umezungumzia dunia nyingine ama uwanda mwingine wa kiteknolojia usiokuwa na pungufu,nikimaanisha kupitia internet ni karibu kila kitu ukitafutacho basi unaweza kukipata. Ila unapozungumzia mitandao ya kijamii hapa tunazungumzia vijisehemu vya internet vinavyotutenganisha na kutuweka katika makundi, hapa ninamaanisha kuwa mitandao ya kijamii, hiki ni kipengele kinachotukusanya na kutuweka pamoja hata kama hatuko mahali pamoja, kwa mfano mimi nawewe tunaweza kuwasiliana kupitia facebook na mitandao mingine bila ya kuonana kabisa, nap engine tukafikia hatua ya kufanya biashara pasipo kuwa karibu. Wapo waliotumia mitandao ya kijamii na internet vibaya wakaambulia vilio, lakini wapo vijana walio itumia fursa hii na kutengeneza pesa kubwa sana, leo nakuletea wachache tu kutoka hapa kwetu Tanzania. Millard Ayo. Millard ni miongoni mwa wanahabari vijana wenye majina makubwa ndani na nje ya Tanzania, kijana huyu ni maarufu sana kupitia vipindi anavyoendesha redioni na pia kwenye televisheni, anataaluma ya uandishi wa habari, na amewahi kufanya kazi na vituo kadhaa vya redio hapa nchini pasi na malipo yoyote. Alikuwa akitafuta nafasi ya kujulikana na kutengeneza pesa kupitia jina lake, millard ayo ameweza kuomba kazi na kunyimwa pasi na sababu yoyote katika kituo Fulani cha habari lakini leo hii kituo hicho kinajaribu kumuwinda kwa nguvu. Millard Ayo, baada ya kufanikiwa kupata kazi clouds fm, alikutana na baadhi ya watu waliomshauri kuwa angeanzisha blog ama website ili atengeneze pesa kupitia habari zake, lakini millard alikuwa mgumu kuamini kama anaweza kufanikiwa kwa njia hiyo. Kwa mara ya pili tena Millard Ayo alikutana na Hissa Michuzi, naye alimshauri kuwa afungue blog au website ili atengeneze pesa kupitia blog yake, Millard alishawishika na akaamua kuanzisha website ya Millard Ayo lakini pia akaanzisha youtube account iitwayo Ayo tv na vyote kwa pamoja alivitumia kutangaza habari. Hivi sasa tunavyoongea Millard ni miongoni mwa vijana wanaotengeza pesa ndefu kupitia mitandao ya kijamii na internet pia, hivi sasa Website yake inatembelewa na watu zaidi 30000 kwa siku na ameshaajiri watu zaidi ya kumi. Asha Abbas Apps and Girls ni taasisi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa na vijana ili kuwapa ufahamu mabinti waweze kuwa na uelewa juu ya maswala ya teknolojia kupitia Programing (kutengeza Program) au coding (lugha siri za kompyuta) ili waweze kundoa woga na kujiajiri kupitia teknolojia. Asha Abbas ni miongoni mwa matunda ya Tasisi hiyo, ni kijana mdogo na mwanafunzi wa shule moja ya sekondari jiji dare s salaam. Binti huyo baada ya kupata fursa ya kupata mafunzo kutoka kwa Apps and Girls aliamua kutengeneza mfumo wa kielektroniki unaowakutanisha vijana wa kitanzania pamoja na washauri wa afya ili kujadili maswala mbali mbali ya afya na jinsia. Mfumo huu unaofahamika kama Aurateen umekuwa ni fursa kubwa kwa vijana wa kitanzania kupata mafunzo ya kiafya. Mfumo huu unamruhusu kijana ama mtu yeyote kuuliza swali na likajibiwa na wataalamu waliobobea katika sekta husika. Asha Abbas amefanikiwa kuwa mfano mkubwa kwa mabinti wa kiafrika hususani Tanzania wanaopenda kupoteza muda mwingi kwenye mitandao huku wakifuatilia mambo yasiyo na manufaa kwao na kwa jamii inayo wazunguka. Asha Abbas amefanikiwa kuanzisha taasisi ya Aura Teens ambapo wanatoa elimu ya afya kwa njia ya mitandao, lakini pia wamekuwa wakizunguka mashuleni kuongea na vijana kuhusu maswala mazima ya maendeleo kiafya na kiuchumi pia, na kwa sasa Asha Abbas ni C.E.O wa Aura Teens. www.aurateens.org Asha Abbas amefanikiwa kutunukiwa tuzo ya Malkia Wa Nguvu mwaka huu. Funzo Vijana tunapaswa kubadirika na kuchangamkia fursa iliyopo ndani ya internet na mitandao yoote ya kijamii,ila pia tusisahau kutilia nguvu katika maswala yanayotuhusu na yanayotupasa kufanya huku tukimtanguliza Mungu. Imeandikwa na L.A.Mugisha email Lamugisha045@gmail.com Phone 0742569200

Comments