HADITHI:MAMA MWENYE CHONGO

Mama mmoja alibahatika kuishi na kijana wake mmoja baada ya mumewake kufariki na kumuacha akiwa na mtoto mchanga. Baada ya kukuwa ,mtoto Yule alianza shule vizuri na akawa mtiifu sana kwa mama yake mzazi na hata jamii nzima. Kijana huyu alipenda sana michezo lakini kunakitu kilimfanya asipende sana kucheza na wenzake, kwani kila alipokwenda kucheza na wenzake basi wale wenzake walikuwa wakimdhihaki na kumcheka kwakuwa mamayakeanajicho moja. Mtotoyule alichukia sana hali iliyopelekea akaanza kumdharau mama yake,”najutakuwa na mama kama wewe mwenye jicho moja” alimwambia hivyo mamayake. Yule mama hakuchukia bali aliendelea kumpenda sana mwanaye, siku ya siku Yule kijana aliamua kwenda zake mjini na kumuacha mamayake akiwa pekeyake akidai kuwa hawezi kuishi namama mwenye jicho moja, mama alimlilia sana mwanaye lakini yale machozi yake hayakuleta faida yoyote. Siku zilipita nyingi, Yule kijana ameshapata mali huko mjini, ana mke na watoto. Basi Yule mama akaamua aende mjini akamuone mwanaye na wajukuu wake, mama kajikoki kabeba vyakula na matunda tele ili apelike kama zawadi, lakini cha ajabu alipofika mwanaye alimtimua na kumwambia kuwa hataki kuwa na mama mwenye jicho moja, Yule mama alilia sana ,kisha alipanda gari na kuondoka. Yule kijana alipokuwa akifunga mlango baada ya kumfukuza mamayake ndipo aligundua kuwa kunabarua mama yake alikuwa ameidondosha chini, Yule kijana aliichukuwa na kuanza kuisoma. Barua ilisema hivii……… “MWANANGU NAJUA UMECHUKIA SANA KUWA NA MAMA MWENYE JICHO MOJA, LAKINI LEO NAOMBA NIKUPE SABABU YA MIMI KUWA HIVI, MWAKA 1988 MIMI WEWE NA BABAYAKO TULIPATA AJARI MBAYA YA GARI WAKATI TUKITOKA SAFARINI, BABAYAKO ALIKUFA HAPOHAPO, WEWEUKATOBOLEWA JICHO LA KUSHOTO NA VILE VIOO VYA GARI NA JICHO LIKAPOFUKA, HIVYO BASI KWA MAPENZI YANGU YA DHATI NILIRIDHIA KUTOA JICHO LANGU MOJA ZIMA ILI UWEKEWE WEWE ILI UPATE KUONA VYEMA.NISAMEHE SANA KAMA NILIKOSEA KUTENDA HIVYO” Kijana alilia sana huku akijilaumu kwa aliyomfanyia mama yake, kwa haraka haraka aliingia ndani ili achukue funguo za gari amfuate mama yake kijijini na kumuomba msamaha, lakini ghafla aliona kwenye tv gari alilokuwa amepanda mama yake likiteketea kwa moto na watu wote waliokuwamo wamethibitishwa kufa. FUNZO MZAZI WAKO HATA KAMA ANAFUNZA USONI, BADO ITAKUPASA KUMHESHIMU MAANA UKO MAHALI ULIPO KWA MSAADA WAKE.

Comments