KILIMOBIASHARA: MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA KUANZISHA BIASHARA.

Mambo ya kuzingatia katika wazo la biashara (a) tambua changamoto, kabla hujaanza jambo lolote lile kwanza fanya utafiti wa kutosha juu ya wazo ambalo ungependa kulitumia ili liweze kukuletea faida (b) Orodhesha mahitaji ya wazo lako, zingatia mahitaji ya wazo lako kwa kuangalia upekee wa biashara yako huduma utakayo kuwa unaitoa kwa kiwango gani,walengwa ni wakina Nani, tambua jinsi ya kumvutia mteja badala ya bidhaa nyingine (c) Mbinu za kukuza biashara yako, kuwa na mikakati na malengo ni jinsi gani utaweza kukuza biashara yako kwa kutafutia njia sahihi au jinsi gani mteja wako au walengwa wa biashara yako wataweza kupata huduma ili ikue kwa kusambaa na kupata masoko sehemu mbalimbali changanua ni jinsi gani utawafikia wateja wako na jinsi gani watajua biashara yako (d) ufanisi wako katika biashara,fanya tathmini ya kiwango cha elimu uliyonayo na uzoefu unaofanana na wazo la biashara na wadau wanaousiana na wazo lako la biashara kama mjasiriamali,,.kujua mbinu mbalimbali za kilimo tembelea tovuti ya WWW.KILIMOTANZANIA.COM

Comments