Mwalimu mmoja wa Somo la Sayansi katika Shule ya Msingi
Mtakuja alijikuta katika mdahalo mkubwa baada ya kutofautiana kifikra na
mwanafunzi wake. Hii ilijitokeza baada ya Mwalimu huyo kufundisha uwepo wa
sayari tisa na kuthibitisha kuwa ndani ya sayari zote zilizobainishwa
kijeografia, Dunia iko moja tu.
“wanafunzi wangu, nataka mjue hili, yapo mafundisho mengi
yanayoonyesha kuwa kunauwepo wa Dunia nyingine. Binafsi nisingependa mshikamane
sana na mafundisho hayo mpaka yatakapokuwa yamethibitishwa.” Alisema Mwalimu
Yule huku akigeuka kumtizama mwanafunzi aliyekuwa akinyoosha mkono ishara ya
kuomba kuchangia mada.
“eeh, Juma unalipi la kuongea , au unaswali”alisema mwalimu.
“hapana mwalimu mimi sina swali ila ninataka kujenga hoja
kuthibitisha kuwa kunauwepo wa Dunia zaidi ya moja”alisema Mwanafunzi Juma.
“kijana usijichanganye,nakupa nafasi ya kuchangia lakini
usije ukathubutu kusema kuwa kuna Dunia zaidi ya moja kwenye Mtihani”alisema
Mwalimu.
“Mwalimu, kijeografia ni kweli kwamba Dunia iko moja tu ,ila
kimantiki ninadhani Kuna Dunia zaidi ya moja”alisema Juma.
“hebu tuelezee”alisema mwalimu.
“Mwalimu, Dunia ya pili ninayoisema watu wakaao ndani yake
kwa asilimia kubwa ni watu wanaoishi maisha yasiyo yao,huko watu hawazaliwi
bali wanajisajili ili kuweza kuishi. Watu wanaishi kwenye Dunia hiyo kutegemea
uwepo wa Dunia hii tunayokaa, nikimaanisha bila ya uwepo wa Dunia hii basin a
Dunia yao isingekuwepo. Cha kushangaza ni kwamba hata majina wanayotumia
Duniani huko sio majina halisi waliyopewa na Wazazi wao,kama huku kwenye Dunia
yetu mtu anaitwa Denis Kezirahabi Machovu, basi kule atajiita DK. Machovu jr.
Kwenye Dunia hiyo karibia kila mtu anamiliki kampuni maana ukitizama usajili wao
utakuta kila mtu kwenye nafasi ya kujaza kazi anayoyanya utakuta ameweka yeye
ni C.E.O mahali Fulani. Katika Dunia hii pumzi inayohitajika ni Data zako tu,
vinginevyo utajua tu mtu Fulani kaongea neon Fulani bila kuona nyuso yake. Huko
nako kuna maofisi kwani watu wa Dunia yetu hii wameingia huko na kuamua kufanya
biasharakwenye ulimwengu huo mwingine”alisema Juma na kisha akaketi.
Wanafunzi wengi walimpigia makofi huku wakistaajabu juu ya
weledi wake wa kutumia fasihi ili kuonyesha ujumbe alionao.Mwalimu naye alibaki
ameduwa kwani alishangazwa sana na ujumbe ule kwakuwa hata yeye kwenye Dunia
hiyo nyingine anajulikana kama mmiliki wa kampuni Fulani kitu ambacho si kweli,
Mwalimu alitoa noti ya shilingi Elfu Kumi na kumpatia Juma kama zawadi huku
akimsihi asitumie Nadharia ile katika sehemu yoyote ihusianayo na masomo yake.
Imeandikwa na Lameck Mugisha
Comments
Post a Comment