
Baba mmoja alikuwa akipenda sana kucheza karata na mwanae pindi wamalizapo kufanya kazi zao za asubuhi. Kutokana na uzee wa Baba, Yule ustadi wake katika mchezo wa karata ukawa ukipungua siku hadi siku, na sikumoja wakati akiendelea kucheza karata na Mwanae, Yule Baba akamuuliza Mwanae, “Mwanangu,hebu niambie ni karata gani unaipenda kuliko zote tangu umeanza kuujua huu mchezo?”. Yule kijana alicheka kidogo kisha akamuangalia Baba yake na kumjibu kuwa aliipenda karata yenye picha ya jokeri. Lile jibu lilimchekesha sana Yule mzee, alimshika bega kijana wake na kisha akamwambia “Mwanangu, hebu nieleze kwanini unapenda sana karata ya jokeri”. Yule kijana alikuna kidogo kidevu chake, akamtazama Babayake na kumjibu kwamba anapenda karata ya jokeri kwani ni kinga ya ushindi wake, naakaongezea kuwa karata hiyo hufichwa kibindoni ili mpinzani wako akaribiapo kupata ushindi basi unaitoa ili kumuongezea vikwazo.Baba Yule alicheka sana na kisha akamwambia mwanae “ umenena vyema kijana wangu, hebu niulize na mimi napenda karata gani”. Yule kijana alimtazama babayake na kisha akamuuliza ni karata gani anaipenda, Baba naye akajibu kuwa anapenda karata ya jokeri,alimuangalia mwanae machoni na kisha akamwambia, “Mwanangu, karata ya jokeri pindi utakapoificha ili uniadhibu nayo pindi ninapokaribia kupata ushindi utakuwa hujafanya maamuzi sahihi,ukinipa karata yenye jokeri utakuwa umeniongezea wingi wa karata na hivyo kunipa njia mbadala ya kuufanya ubunifu ili niufikie ushindi wangu”, kijana alishangazwa sana na jibu la Babayake na kujikuta akiwa amepata funzo kubwa maishani mwake.
FUNZO
MPINZANI WAKO ANAPOKUPA MAJARIBU DAKIKA ZA MWISHO KABLA YA KUUFIKIA USHINDI KATIKA MAISHA YAKO, NI SAWA NA KUTILIA MAJI KATIKA MMEA ULIONYAUKA,USIOGOPE WEWE SONGA MBELE.
IMEANDIKWA NA
L.A.MUGISHA.
Comments
Post a Comment