Sura na muonekano
wake ni mithiri ya mtoto mtulivu sana, najua wengi kwakumuona na bila ya
kumfahamu usingewezxa kudhani kama anauwezo wa kuruka japo kwa umbali wa
sentimita moja kwenda juu. Si wa kujiweka sana ukurasa wa mbele, bali kazi na
maajabu anayofanya kwaajili ya taifa lake ndivyo vinavyo mfanya afahamike sana
hapa kwetu Afrika mpaka Mabala ya nje.
Wendy Waeni ni
Mwanasarakasi mdogo kutoka nchini Kenya, inasemekana kwa wengi kuwa pengine
ndiye mwanasarakasi mdogo zaidi Afrika mwenye jina kubwa ndani na nje ya Bara
la Afrika.Wendy Waeni hadi alipofikisha miaka kumi tayari alikuwa amekwisha perfom mbele ya
maraisi wengi sana kutoka ndani na nje ya Afrika,Paul Kagame, John Mahama,
Uhuru Kenyata na David Cameron ni Miongoni mwa viongozi ambao Wendy amewahi
kuwaonyesha kipawa alichonacho cha kucheza sarakasi.
Uwezo wa Wendy
ulianza kuonekana tangu akiwa Mdogo sana, na kwa wanaomfahamu wanasema alikuwa
akifanya michezo ambayo iliwatisha wengi hususan mama yake mzazi. Mtoto huyu
kipaji chake kiliendelea kukua siku hadi siku hali iliyopelekea kujiunga katika
kikundi cha HURUMA, kinacholea vipaji vya aina hiyo.
Baada ya Wendy
kujiunga katika kundi hilo lililokuwa likiitwa kwenye maonyesho kadha wa kadha,
ndipo taifa la Kenya lilipomtambua na kuona uwezo aliokuwanao mtoto huyu kwani
amekuwa kivutio kwa wengi pindi alipofanya maonyesho katika sherehe nyingi za
kitaifa.
Siku kadhaa
zikapita, Jeff koinange pamoja na Television nyingi kutoka Kenya zilizizima kwa
uwezo aliokuwanao binti huyu, interviews nyingi zilipelekea Wendy Waeni
kujulikana mpaka kimataifa. Lakini kati ya ndoto alizo kuwanazo, ni kufanya
maonesho mbele ya Rais wa Rwanda Paul Kagame, na ndoto yake ilitimia miaka
miwili baadaye ambapo alialikwa na Rahis huyo kwenda white house ya Rwanda.
Hatimaye ndoto
yake ikatimia, na hakuishi tena ndani ya ndoto, bali aliutembelea uhalisia
wake.
Imeandikwa na
L.A.Mugisha
0742549200
Comments
Post a Comment