OCHU KIOTA:NATENGENEZA VIDONDA ILI NIPATE KUISHI

  Inawezekana kabisa Ochu Kiota si jina geni saana kwa waaandaaji wa filamu ndani na nje ya Tanzania,inawezekana jina hilo linakuletea mandhari ya raia wa nigeria kutokana tu na majina tuliyozoea kuyasikia katika filamu za Nijeria.

  kwa muonekano wake akiwa kazini,unaweza kufikiri ni mganga wa kienyeji kutokana na vifaa vinavyokuwa vimemzunguka wakati akifanya kazi yake ili apate kula,laa hasha Ochu ni mmoja wa kijana aliyeamua kutazama fursa ndani ya tasnia ya filamu na kuamua kuifanyia kazi. Katika tasnia ya filamu hapo nyuma kulikuwa na ukosefu au mapungufu katika nyanja mbalimbali, ali kadhalika ukosefu wa uhalisia ilikuwa ni miongoni mwa changamoto zilizoikumba tasnia ya filamu. Mazingira kama vile,mtu kuungua, mtu kapata ajari, au mtu kachomwa kisu yalikuwa yanafanya filamu za Kitanzania zionekane hazina uhalisia kwani watu walitumia ubunifu mdogo kutengenezamazingira hayo.

  Ochu Kiota aliona fursa kubwa katika utengenezaji wa mazingara yasiyo ya kweli na kuyafanya kuwa ya kweli,alianza kwa kutengeneza vinyago kwa kutumia taka na vitu vingine vilivyopelekea unadhifu wake kuwafikia hadhira, muda ulipita na hatimaye akafanikiwa kuongeza ubunifu wake na kuanza kutengeneza vidonda katika miili ya wasanii ili dhima yao iweze kuwafikia hadhira kwa uhalisia wake.Mpaka sasa Ochu amefanikiwa kufanyakazi na wazalishaji wengi wa filamu kama vile L.P MEDIA na wengine kadha wa kadha. 

picha na vielelezo

Ochu Kiota*halisi*

moja ya kazi alizofanya

Hapa anajaribu kuitengeneza sura ili awe na muonekano kama wa mtu mwenye ulemavu wa ngozi.


 

Comments