MADAM AKIWASHA TENA INSTAGRAM

MADAM AKIWASHA TENA INSTAGRAM. Muigizaji kutoka Bongo muvi na aliyewahi kuwa Miss Tanzania, Wema Sepetu amezidi kuwa gumzo mitandaoni baaada ya kimya cha muda mrefu katika kazi zake. Gumzo lililoamsha hisia za watu wengi walioonekana kuwa upande wa bibie Wema, ni baada ya mrembo huyo kupost picha ya muigizaji mwenzie Esha Buheti iliyomuonyesha kuwa ni mja mzito na kisha akaandika ujumbe mzito uliuosomeka hivii….. Wema Sepetu “yaani ni hivi, hakunaga jipya now mwaweza nitukana nikashituka maana mimi mwenyewe nishajikubali hali yangu…. Labda niulize tu, Niko pekeyangu nilokosa mtoto au ambaye sijazaa….? HAPANA sooo Back to the main point, Nilichosema na nitakachoendelea kusema, MUACHE KUTUWEKEA MIPICHA YA MITUMBO YENU YENYE MISTARI WA UJAUZITO… Yaani inshort muache kupiga picha za UTUPU kwenye maternity shoot zenu…. @esha.s.buheti Nakupenda mama… you’re the definition of womanhood&motherhood na unajua utamaduni wetu nini unataka…. Haya wazungu endeleeni na uzungu wenu ….tukaneni na hapa pia… Eti u thought I would keep quite jus cause mmeniita jina nililozoea so nisi speak my heart…Y’all are very funny…!!! Allah akutangulize kipenzi change…Baby shower loading…. Nakisha akamalizia kwa kumtagg eshabuheti. Kilichowasisimua wengi ni jinsi Mrembo huyo alivyowafunga midomo watu kwa ujumbe huu, wengi walimsupport hali iliyopelekea timu pinzani kutokomea vichakani hukooooo. By Lameck Mugisha.

Comments